“Baba Diamond ni mgonjwa kwa muda mrefu sana lakini Diamond hajawahi kuja kumuona hata siku moja,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, waandishi wetu walifunga safari mpaka nyumbani kwa mzee huyo, Magomeni-Kagera, jijini Dar ambapo alikiri kuugua kwa muda mrefu na kukosa msaada kutoka kwa Diamond.
“Nasumbuliwa na miguu kwa muda mrefu sana na ninatibiwa katika Hospitali ya Saint Monica, Manzese-Darajani. Diamond ana taarifa za kuumwa kwangu lakini hajawahi kuja kuniona.
“Namshukuru mwanangu Queen Doreen kwa kunijali kwa kila kitu,” alisema baba Diamond.
No comments:
Post a Comment