Contacts

Thursday, September 26, 2013

AJALI MBAYA ASUBUHI HII

HIVI NDIVYO AJALA MBAYA ILIVYOTOKEA LEO ASUBUHI BARABARA YA MAJITA KARIBU NA MAKAZI YA MKUU WA MKOA,KUMRADHI KWA PICHA






                                   ASKARI WA USALAMA BARABARANI WAKITOA MSAADA



 
Ajali mbaya imetokea asubuhi ya leo majira ya saa 2 kwenye barabara ya majita karibu na makazi ya mkuu wa mkoa wa Mara baada ya gari aina ya VX land cruser namba T 901 AHH kuigonga pikipiki iliyokuwa ikitoka maeneo ya mjini musoma kuelekea kamnyonge.
 
Kamera yetu imemshuhudia majeruhi wa ajali aliyedaiwa kuwa ni abiria akiwa anavuja damu nyingi kichwani huku akipumua kwa shida na muda mchache askari wa kikosi cha usalama barabarani walifika eneo la tukio na kumchukua kwa ajili ya kumuwahisha hospitali.
 
Mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo kabla ya camera ya bloog hii kufika eneo la tukio muda mchache wamesema dereva wa pikipiki ambaye alidaiwa kupakia abilia alitaka kulipita gari hilo na kuingia eneo la gari hali iliyopelekea kutokea kwa ajali hiyo.
 
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo dereva wa pikipiki Wambura Matiku aliyekuwa nyuma ya pikipiki iliyopata ajali aliiambia blog hii dereva wa pikipiki mara  baada ya kulipita gari hilo aliwahi kuingia upande wa gari na kutokea kwa ajali hiyo.
 
Hata hivyo jeshi la polisi mara baada ya kumuwahisha majeruhi huyo hospitalini walirejea eneo la tukio na kupima ili kubaini chanjo cha ajali hiyo huku Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara Ferdinand Mtui akiahidi kuhitolea taarifa mara baada ya kubaini chanzo cha ajali hiyo

Monday, September 23, 2013

GARI INAUZWA USED CAR GOOD CONDITION GX 100 T734 BMR

                                                      CONTACT 0652489648

Thursday, September 12, 2013

TALK OF THE WEEK BY HUSSEIN KOVA

HUSSEIN KOVA ATOA USHAURI KWA VIJANA WENZAKE KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII.

Hussein Kova pichani juu aonesha mfano wa kuigwa awaasa vijana wenzake kuepukana na vishawishi vya kujiingiza kwenye majanga ya biashara haramu ya madawa ya kulevya.
soma hapo chini alicho kiandika kwenye kurasa zake za instagram na facebook.

Sunday, September 8, 2013

M23 WANAKUBALI KIAINA YAKE DRC CONGO

M23: "TUPO TAYARI KWA MAZUNGUMZO,VITA...."


                Kiongozi wa waasi wa M23, Bertrand Bisimwa

WITO uliotolewa na viongozi wa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu wa kuitaka Serikali ya Kongo ikae meza moja na waasi wa M23 kwa ajili ya kutatua mgogoro wao, umepokewa kwa mikono mwili na waasi hao, ingawa wametoa angalizo la kurudi tena kwenye uwanja wa mapambano iwapo watachokozwa.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili kwa njia ya simu, kiongozi wa kundi hilo la waasi wa M23, Betrand Bisiimwa, alipongeza uamuzi huo wa kuwataka wakutane na Serikali ya Kongo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mgogoro wao ambao umedumu kwa muda mrefu.

Bisiimwa akizungumzia uamuzi huo uliofikiwa hivi karibuni katika kikao kilichoketi Uganda, kilichowashirikisha Rais Jakaya Kikwete, Paul Kagame wa Rwanda, Joseph Kabila wa Kongo, Yoweri Museveni wa Kongo na wengine, alisema kikundi chake kilifanya juhudi kama hizo kwa zaidi ya miezi kumi iliyopita, lakini serikali ya Kongo iliwapuuza, hivyo kusisitiza kwamba wapo tayari kwa mazungumzo au kuendelea na mapigano.

Naupongeza wito wa viongozi wa Nchi za Maziwa Makuu kwa sababu wameona umuhimu wa kuyaokoa maisha ya Wakongomani wa hapa mjini Goma, siku zote amani inatafutwa kwa makubaliano ya kukaa meza moja, lakini ukiamua vita hauwezi kushinda,” alisema Bisiimwa.

Wakati Bisiimwa akitoa kauli hiyo, siku chache zilizopita alikaririwa na gazeti dada la MTANZANIA Jumatano akikiri kuwa majeshi ya Umoja wa Mataifa ni hatari na yanaweza kuwamaliza.

Hivi karibuni viongozi wa nchi zinazounda Ukanda wa Maziwa Makuu ulitoa wito wa siku tatu kwa Serikali ya Kongo kukutana na waasi wa M23, ili kujadili njia zitakazoleta amani katika eneo la Mashariki mwa Kongo.

Rais wa Uganda, Museveni, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo, ameelezea uwepo wa nafasi kubwa ya kufikia makubaliano ya kumaliza mapigano kati ya pande zote mbili.

Mbali na hilo, MTANZANIA Jumapili ilipomtaka athibitishe kama wapiganaji wake wapo tayari kusalimisha silaha, alikataa na kusema wapo tayari kwa vita.

“Jeshi langu limerudi nyuma tena kwa kilomita mbili kutoka mji mdogo wa Kanyaruchinya kwa lengo la kurejesha amani katika mji wa Goma na pia kupisha uchunguzi wa makombora yaliyotokea katika mji huu na nchi ya jirani ya Rwanda, sasa kama wakitufuata huku kwa ajili ya vita tutapambana nao, na kama ni mazungumzo ya amani basi ninaunga mkono hilo,” alisema.

Wakati kiongozi huyo wa M23 akisema hayo, zipo taarifa zinazodai uamuzi wa waasi hao kurudisha nyuma vikosi vyake unatokana na kipigo kikali walichokipata katika mapigano yaliyotokea katikati ya wiki iliyopita, kutoka kwa kikosi cha FIB ambacho kipo chini ya jeshi la kulinda amani la MONUSCO, kikiongozwa na askari wa JWTZ.

Habari ambazo zimenaswa na gazeti hili zinasema kuwa jeshi la MONUSCO imefanikiwa kuchukua umiliki wa mji wa Goma kwa asilimia 95, huku kikosi cha askari wa Serikali ya Kongo wanaoshirikiana na FIB wakitangaza nia ya kuendeleza mapigano dhidi ya waasi wa M23, kwa lengo la kuwapokonya silaha.

-Mtanzania