Contacts

Wednesday, May 29, 2013

PICHA YA NGWEA AKIWA MOCHUARI SOUTH AFRICA

NIMEPATA BAHATIYA KUHAKIKISHA PICHA YA MAREHEMU ALBERT NGWEA IKIWA MOCHWARI SOUTH AFRICA ASANTE SANA KWA FADDY DE DON ALIYEKUWA SOUTH KWA KUNITUMIA HIIPIC KUWAONYESHA WATANZANIA WENZANGU.MAY GOD REST HIM IN PEACE.AMEN

Tuesday, May 28, 2013

KILOCHOMUA NGWEA INCHINI SOUTH AFRICA (R.I.P ALBERT NGWEA)

HIKI NDICHO KILICHOMUUA NGWEA

Habari kutoka kwa mtu wa karibu na Rapper Ngwea, aliejitambulisha kwa jina la Hamisi, amesema Ngwea alikua kule kwa mualiko wa kufanya show South Africa, ambapo alikua na msanii mwingine anaeitwa M to the P, na walitakiwa kuondoka leo kurudi Dar saa tatu asubuhi, lakini baada ya kuona hawatokei ndio wakaamua kwenda walipokuwa wamefikia na kuwakuta wote wawili wakiwa hawajielewi baada ya kujidunga madawa ya kulevya mengi (overdose), walipowahishwa hospitali, habari ndio ikawa hivi, kuwa Ngwea amefariki na M to the P yuko hoi hospitali
May God give you peace brother.

Monday, May 27, 2013

BANDARINI FURSA SASA KWA OUR COMPANY (FREIGHT REACH SERVICES)

WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO WAKUTANA KUZUNGUMZA KUHUSIANA NA MIZIGO YAO ILIOKWAMA BANADARINI

Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo wameahidi kuendelea kutafuta suluhu kwa njia ya mazungumzo na serikali juu ya mgogoro wa makontena ambayo yamezuiliwa bandarini, kitendo ambacho kimeathiri biashara zao kwa mda mrefu sasa kwani wemeshindwa kufanya biashara ndani na nchi jirani kwa takriban zaidi ya wiki tatu.

Tamko hili lililotolewa na Jumuiya Hii wiki iliopita, limeeleza kuwa tayari wametuma maombi kwa wizara husika na idara za serikali za mapato ili kuwepo na mkutano utakaoweza kutizama jinsi ya kutatua mgogoro wa makontena zaidi ya 400 ambayo yamezuiliwa bandarini.

Katika tamko hilo imeelezwa kuhusu dhamira yao ya kukutana na Waziri wa Fedha na Uchumi, Waziri wa Viwanda na Uwongozi wa TRA pamoja na vyombo vingine husika ili kujadili na kutafuta ufumbuzi wa kile wanachodai ni ongezeko la kodi.

Wanasisitiza kuwa kuwepo kwa pande zote hizi kwenye mkutano kutawezesha kufikia ufumbuzi.

Jambo lililopelekea kufikia uamuzi huu wa kukutana na viongozi ni kile walichokiita kutekwa nyara kwa kikao cha awali kilichofanyika na Waziri wa Fedha ambapo Chama cha Mawakala wa bandarini kilifunika nafasi hiyo kwa kujadili matatizo yao wenyewe bila ya kujali kero inayowakabili wafanyabiashara ambao tayari wameanza kupata hasara kutokana na makotena yao kukwama.

Wafanyabiashara wamelalamika juu ya mawakala kuingia katika malumbano yao binafsi juu ya ushindani wa kibiashara badala ya kutafuta suluhisho la makontena yalio na bidhaa za wafanyabiashara hawa wadogo wadogo.

Hata hivyo tamko la wafanyabiashara limeweka wazi kuridhika kwao na maelekezo yaliyotelewa na Waziri wa Fedha na maafisa wa TRA juu ya kukubali kwao kufanya kikao haraka na wafanyabiashara hawa.

Wafanyabiashara pia wametakiwa kujaza fomu upya ambazo zitaeleza upya aina za bidhaa walizoleta nchini na vielezo kamili vya bidhaa hizo ili vifanyiwe uhakiki upya.

Pia wamehakikishiwa kuwa hawatatozwa faini kwa makosa yoyote yatayobainika baada ya kuhakiki fomu zao upya, iwapo zitakuwa na dosari. 

Jumuiya hiyo pia imesema kwamba iwapo kulikuwa na ukwepaji wa kodi basi badala ya TRA kuwaadhibu wao nivema wangechukua hatua dhidi ya wale wote waliokwenda kinyume.

Katika malalamiko yao wanadai kuwa ushuru wa forodha (Import duty) na VAT zimeongeka mara mbili bila ya wao kupewa taarifa.

Pia wanadai kuwa TRA haikufuata utaratibu katika kuongeza kodi.Wanadai pia wafanyabiashara wanalalamika juu ya HS Code ambayo inatumika kuonyesha aina ya bidhaa mbali mbali na ushuru wake kwa madai ya kuwa imechakachuliwa.

Lakini wafanyabiashara wameendelea kusisitiza kuwa wao ni wananchi wenye kutii sharia za nchi na wako tayari kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili katika meza ya mazungumzo.

Wameelezea jinsi walivyoanza kupoteza wateja wao mara baada ya mizigo yao kuzuiliwa bandarini, ikiwa ni pamoja na usumbufu mkubwa kwa wateja wao ambao wanatoka katika nchi za Afrika mashariki na nyinginezo.

Wamesema hivi sasa kuna uwezekano wa wateja wao kuhama na kufanya biashara nchi nyingine jambo ambalo litaipotezea taifa kiwango kikubwa cha pato la taifa.

Wafanyabiashara hao wanadai kuwa tayari wapo wenzao ambao wamekufa kutokana na kutetereka kwa biashara zao baada ya kuambiwa walipe kodi kubwa ambayo imewaletea mshituko mkubwa hadi kufikia kupoteza maisha.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na jumuiya, tayari mali ya mabilioni imekwama na gharama za kuukomboa zinaongezeka.

Sunday, May 26, 2013

BIG BROTHER AFRICA 2013

FEZA KESSY NA NANDO WAIWAKILISHA TANZANIA NDANI YA BBA 2013




Big Brother Africa  2013 "The Chase" imeanza kwa kasi usiku wa leo (26 may) na msanii Feza Kessy na Nando ndio wanaoiwakilisha Tanzania. kwa mujibhu wa story yake mwenyewe Nando ni mtanzania anaeishi marekani lakini ilimbidi aombe hela kwa marafiki zake kwa ajili ya kupata ticket ya kuja Tanzania kufanya usahili wa BBA, amesema kama angekosa nafasi ya kuiwakilisha Tanzania asinge juta maana pia alikua hajamuona bibi yake kwa miaka mingi, kwahiyo angekuwa kaitumia nafasi hiyo kuja kumuona bibi yake.

Thursday, May 23, 2013

KIMENUKA MTWARA

MTWARA : GESI GESI WAR UPDATE

  •  Mabasi 5 ya Champion yamebeba Wanajeshi yako njiani yanakuja.
  •  Serikali yatoa tamko yasema watu 91 wanashikiliwa.
  • Bunge laahirishwa tena. Kupisha uchunguzi na kuepusha uchochezi kutoka kwa baadhi ya wabunge. (Kwa mujibu wa Spika)
  •  Maeneo ya Magomeni, Chikongola, Nkanaledi, Mikindani  maaskari wanaingia majumbani mwa watu na kumsomba mtu yeyote ambaye ni mwanaume awe amehusika awe hajahusika na kumkamata. Pia inaripotiwa na uhalifu unafanywa na maaskari hao hao.  Jambo linaloamsha hisia kwa wananchi.
  • RPC anaongea na vyombo vya habari na kuwasihi wananchi waende makazini. Lakini kiuhalisia hali sio shwari.
  • Mahakama ya mwanzo ya Mitengo imechomwa moto
  • Mpaka sasa ni vita baina ya wananchi na maaskari. Mabomu yamesikika pamoja na milio ya risasi masaa 24. Na milio ya Risasi na mabomu inaendelea kusikika.
  • Raia wapatao 7 wameripotiwa kufariki (wengine walipelekwa hospitali ya Ndanda Ndogo na mmoja ameripotiwa kupokelewa Ligula.
  • Nyumba za viongozi zinaendelea kuchomwa moto.
  • Majibizano baina ya Polisi na Raia yanaendelea maeneo ya Magomeni, Nkanaledi na Mikindani.

  • Maduka yamefungwa na hakuna huduma zozote
  • Barabara zimewekwa vizuizi magogo na matairi yamechomwa moto. Hakuna njia ya kupita.  
 SHUJAA WA GESI ALIYEPIGWA RISASI 
 RIP Kaka Karim(Picha Mpasta, JAMII FORUMS)

Tuesday, May 14, 2013

LIKE FATHER LIKE SON

BABU LOLIONDO

HAYA NDIO MAISHA YA BABU WA LOLIONDO KWA SASA





 
 
Hii ni nyumba aliyokuwa anaishi Babu Ambi kabla Dozi ya Kikombe haijachanganya.
 

Friday, May 10, 2013

MAJAMBAZI TENA KARIAKOO

BREAKING NEWS, MAJAMBAZI YAPORA KARIAKOO NA KUUA MAENEO YA BARABARA YA UHURU

Majambazi yapora mama mmoja kiasi cha shilingi milioni kumi leo na kutokomea kusikojulikana. Tukio hilo limetokea leo saa 5:16 asubuhi, inavyosemekana mdada huyo  alikua akitoka benki ya CRDB tawi la Uhuru ambapo majambazi yakiwa na pikipiki yalikua yakimfuatilia, alipotoka tu wakaligonga gari lake makusudi ndipo dada huyo aliposimama ili angaalie nani kagonga gari yake ambapo jambazi mmoja alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokomea na kiasi hicho cha pesa. Mpaka tunaingia mitamboni hakuna habari yoyote ya kukamatwa kwa wahalifu hao.

Sunday, May 5, 2013

PICHA ZA MAJAMBAZI WALIOUWAWA MBEYA

TASWIRA YA WATU WATANO WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WALIOUWAWA NA POLISI MKOANI MBEYA


Kamanda diwani akiwaonyesha moja ya jambazi lililokuwa limeshika siraha