Contacts

Wednesday, July 31, 2013

"THE CEO" YOUNG MILLIONEA DAVIS MOSHA BATA BATANI MAREKANI

MILIONEA JIMMIE MAGGETTE AMWALIKA DAVIS MOSHA 'THE CEO' KATIKA KUSHEREHEKEA BIRTHDAY YAKE HOLLYWOOD, L.A

Davis Mosha "The CEO", Deo Temba "Mayor wa LA" na milionea Jimmie Maggette wakiwa katika Supper Club Hollywood jana usiku kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa tajiri Jimmie ambaye ni mdogo wa mcheza basketball maarufu na tajiri Corey Maggette. MC wa party alikuwa mwanamuziki maarufu J Cole. Wamarekani weusi wanajisikia proud sana wanapokutana na successful people kutoka Afrika.

The CEO Davis Mosha, D. Temba, Jimmie Maggettte na Alex King

 Deo Temba "Mayor wa L.A." katikati ni Mlinzi (BodyGuard) wa Davis Mosha " The CEO"

Baada ya The CEO Davis Mosha kukubali mwaliko wa Jimmie Maggette alitumiwa mlinzi maalum (Body Guard) wa kumlinda, maana sehemu hiyo hawaendi watu wa kawaida, lazima uwe na mlinzi. Hapa Boss Mosha akiteta jambo na Body Guard wake.

   Mayor wa L.A. Deo Temba akikaribishwa kwenye gari na Boss Mosha

Ricardo Emmanuel Brown Rapper maarufu na aliyewahi kuwa Excutive Vice President wa Death Row records, jina la kisanii  Kurupt aka Kurupt tha Kingpin, aka Kurupt young Gotti au Young Gostra, ni member wa kundi kali la hip-hop la Tha Dogg Pound na HRSMN akiwa na The CEO Davis Mosha katika birthday party ya Jimmie Maggette Super Club, Hollywood Los Angeles.


  Deo Temba "L.A Mayor," Davis Mosha" The CEO" na Comedian Maarufu Funny Man Red Grant

Alex King na tajiri na mmiliki wa Kiota maarufu cha R n B LIVe Hollywood. L.A.

 Bathroom ina kila aina ya perfumes, zote expensive ukiingia lazima utoke na unyunyu mpya na pipi za bei ghali.

 Alex king akiwa na Bodyguard wa Davis Mosha Super club L.A.

Thursday, July 25, 2013

HIVI NDO WALIVYOMWAGIA TINDIKALI MMILIKI WA HOME SHOPPING CENTRE

MFANYANYA BIASHARA MAARUFU WA HOME SHOPPPING CENTRE ALIVYOMWAGIWA TINDIKALI INCHINI AFRICA KUSINI.

Sunday, July 7, 2013

TAMASHA LA MATUMAINI HALIMA VS JACK


PICHA ZA MPAMBANO WA NGUMI WA HALIMA MDEE NA JACK WOLPER





Jana katika tamasha la matumaini Jackline Wolper na Halima Mdee walizipiga ....hapakupatikana mshindi baada ya kutoka Droo

MAPENZI NA CHUO YANAUWA ANGALIA HAPA


MWANAFUNZI WA VETA-DODOMA AJIRIPUA NA PETROLI .....KISA WIVU WA MAPENZI


MWANAFUNZI wa Chuo cha Ufundi (VETA), mkoani Dodoma, Taliki Juma (22), amefariki dunia baada ya kujilipua kwa mafuta ya petroli. Mbali na mwanafunzi huyo kufariki, watu wengine wanane waliokuwa karibu na moto huo nao walijeruhiwa vibaya. 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma na kusainiwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa, David Misime, tukio hilo lilitokea juzi saa 12.30 jioni katika Kitongoji cha Machaka, Kata ya Nzughuni.

Kamanda Misime alisema, katika tukio hilo marehemu alinunua mafuta ya petroli lita tano katika kituo cha mafuta cha Nanenane na kisha kujilipua.

“Juma ambaye ni mwanafunzi wa fani ya ufundi wa magari, alimwaga petroli hiyo ndani ya saluni ya Irene Mapunda na kujilipua.

“Watu waliokuwa karibu naye walijaribu kumsihi asijilipue lakini hawakufanikiwa, kwani aliwasha kibiriti ndani ya saluni hiyo na kusababisha moto mkubwa kulipuka ambao uliwaunguza wengine waliokuwa karibu naye pamoja na mali zote zilizokuwa ndani ya Saluni hiyo.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio hili,” ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo waliojeruhiwa ni Mugina Hessein (32), Benson Mushi (11) Japhet Japhet (18), Meshack John (18), Swaibu Kassim (20),Ester Silau (30), Shaban Pili (20) na Fedrick Gabriel (21).

Majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General) na tathimini ya hasara iliyosababishwa na moto huo bado haijafahamika.