Contacts

Friday, June 21, 2013

KWA MTAZAMO WANGU

NIONAVYO MIMI BUS LA TORRES SIPANDI
Kwenye michuano ya mataifa ya ulaya,TORRES kama masihara aliweza kunyakuwa kiatu cha mfungaji bora na hii hii style yake ya kimagumashi.Mechi nyingi alitokea bechi na bila jasho aliweza kupasia nyavu.
Jana naona tena kaokota WALLET kariakoo baada ya kuwafunga wale DJIBOUT ya Australia TAHITI goli 4 peke yake.Hongera EL NINO lakini hata kama mpira ni magoli bado,Torres hajanishawishi.
kazaliwa 1984 bado naamini anauwezo wa kurudi kwenye form na kuendelea kutamba kama alivyokuwa na Atletico Madrid na Liverpool.Kwa hali hii kama atapata magoli mengine mawili ya kimagumashi,ataibuka tena mfungaji bora.
kwa namna anavyocheza siku hizi,hata kama jana Torres angefunga magoli yote 10,bado ingekuwa ngumu kusema kwamba FERNANDO TORRES is back.Nasikitika kuona tunapata mafungaji bora ambao wenyewe sio bora.

No comments:

Post a Comment