PICHA / MAZISHI YA MFANYABIASHARA BOB SAMBEKE AZIKWA NYUMBANI KWAO MOSHI .
 |
Mwii wa marehemu Bob Sambeke ukiwa kwenye jeneza tayari kwa mazishi |
 |
Jeneza la marehemu Bob Sambeke likwa nje tayari kwa ajili ya kuaga mwli |
 |
Mtoto wa marehemu Jamal akifungua jeneza la marehemu baba yake Bob |
 |
Jamal akiwa ameshafunua jeneza la baba yake |
 |
Watoto wa marehemu Sia na Getrude |
 |
Mwili wa marehemu ukiwa kwenye gari tayari kwa safari kuelekea Moshi kuzika |
 |
Gari liliokuwa limebeba mwili wa marehemu Bob |
 |
Baadhi ya waombolezaji na magari eneo la tukio nyumbani kwa marehemu Njiro, Arusha |
Umati mkubwa wa watu ulifurika nyumbani kwa marehemu “Babu Sambeke”
eneo la njiro jijini Arusha kuuaga mwili wake unaotarajiwa kuzikwa
nyumbani kwake eneo la Karanga mjini Moshi .
Taratibu za kuaga mwili wa marehemu zilianza majira ya saa 5 asubuhi
huku wafanyabiashara wa madini pamoja wafanyabiashara wengine kutoka
Arusha na Moshi wakionekana kutawala msiba huo.
Magari ya kifahari nayo yalitawala na kusababisha msongamano mkubwa kwenye barabara ya Njiro.
Shughuli hizo zilikamilika majira ya saa 8:45 mchana huku mwili huo
ukipakiwa katika gari maalumu la kifahari tayari kusafirishwa kuelekea
nyumbani kwake Moshi kwa ajili ya maziko.
Katika zoezi hilo la kuuaga mwili wa marehemu, Padri Florentine Mallya
ambaye ni mdogo wa marehemu aliongoza misa ya kumuombea marehemu .
Ndani ya jeneza marehemu alivishwa nguo zake za urubani.
Tofauti na ilivyozoeleka katika misiba mingine hapa nchini, katika msiba
huu watu mbalimbali walipata fursa ya kupata chakula na vinywaji
mbalimbali kwa kujihudumia wenyewe, vikiwemo vinywaji aina ya Bavaria
ambapo watu waliohudhuria zoezi hilo walionekana wakijihudumia zaidi
kinywaji hicho.
No comments:
Post a Comment